www.ngonedo.org
Ngo Ngonedo's blog: Mtandao wa Asasi za Kiraia Mkoani Dodoma (NGONEDO) inatekeleza Mradi wa Miaka mitatu (Jan 2015 - December 2017) wenye lengo la kuimarisha Utawala Bora na Demokrasia kwa Viongozi wa ngazi za chini za kiutawala yaani viongzo wa Serikali za Vijiji na Mitaa. Mradi huu ni Matokeo ya Mradi wa Ufatiliaji Matumizi ya Raslimali za Umma uliokwisha mwaka 2013.
Mratibu wa NGONEDO ambae pia ni Mratibu wa Program za Mradi akitoa taarifa za Utekelezaji wa Mradi huo kuanzia mwezi January 2015 hadi June 2015 ameeleza wajumbe wa Mkutano shughuli ambazo zimekwisha kutekelezwa kama zifuatazo;
1. Kutambulisha mradi kwa wadau: Mratibu alieleza kuwa mradi umekwisha Kutambulishwa kwa Wadau katika wilaya zote saba za Mkoa wa Dodoma.
2. Kutoa Mafunzo kwa viongozi wa Serikali za Vijiji kumi na Kimoja vya Wilaya ya Kongwa na Mpwapwa: Idadi ya Viongzo waliopata Mafunzo ni 422 ikiwa Wanawake 109 na wanaume 313.
3. Kutengeneza na Kusambaza vifaa vya Utawala Bora na Demokrasia katika vijiji 11 vya Mradi:
4. Kutengeneza na kusamabaza vifaa vya Elimu Mradi kwa walengwa wa Mradi
5.Kuandaa Matangazo na Vipindi vya redio.
6. Ufuatiliaji na tathmini: Mratibu alifafanua kuwa ufatiliaji uliokwisha kufanywa imeonyesha kuwa uelewa wa viongzo hasa kwenye masuala yanayohusu utawala bora na demokrasia umeongezeka ikilinganishwa na kabala ya Mafunzo
Katika kuhitimisha taarifa yake ya utekelezaji Mratibu huyo wa Mtandao Ndugu Edward Mbogo aliziomba Halmashauri za Serikali za Mitaa kuunga mkono juhudi zilizofanywa katika kukuza demokrasia na utawala bora hasa katika kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Kwa upande wake Mgeni rasmi Bi. Josephine Pamela ambae pia ni Mjumbe wa Bodi ya NGONEDO aliipongeza NGONEDO na Halmashauri zote za Wilaya kwa mapokeo yao ya Mradi huu. Aliwasisitiza Maafisa Maendeleo kutoa ushirikiano mkubwa hasa kwa kuwa Asasi za Kiraia zimebeba jukumu ambalo ki Msingi lilipaswa kutekelezwa na Halmashauri.
Kwa upande wa Washiriki, Ndugu Makundi ambae ni Mratibu wa Mtandao wa Asasi za Kiraia Wilaya ya Chamwino alieleza kufurahishwa na jinsi utekelezaji ulivyo shirikishi hasa kwa kuyafikia makundi yaliyo vijijini. Pia alitoa ushauri kuwa Halmashauri zote zishiriki kikamilifu katika kuifanya Miradi kama hii ili iwe endelevu kwa ustawi wa jamii.
NGONEDO inatekeleza Mradi huu katika wilaya za Kongwa, Bahi, Kondoa, Chamwino, Mpwapwa, Chemba, Kondoa na Doodoma Mjini, Mradi huu unategemewa kuwafikia viongozi takribani 1580 katika vijiji 42 vya mkoa wa Dodoma na wananchi wa kawaida takribani 350,000 kwa kipindi cha miaka miwili.
William Lucas-Afisa Mradi (Mawasiliano)