www.ngonedo.org
Ngo Ngonedo's blog: Mtandao wa Asasi za Kiraia Mkoani Dodoma (NGONEDO) inatekeleza Mradi wa Miaka mitatu (Jan 2015 - December 2017) wenye lengo la kuimarisha Utawala Bora na Demokrasia kwa Viongozi wa ngazi za chini za kiutawala yaani viongzo wa Serikali za Vijiji na Mitaa. Mradi huu ni Matokeo ya Mradi wa Ufatiliaji Matumizi ya Raslimali za Umma uliokwisha mwaka 2013.
Mratibu wa NGONEDO ambae pia ni Mratibu wa Program za Mradi akitoa taarifa za Utekelezaji wa Mradi huo kuanzia mwezi January 2015 hadi June 2015 ameeleza wajumbe wa Mkutano shughuli ambazo zimekwisha kutekelezwa kama zifuatazo;
1. Kutambulisha mradi kwa wadau: Mratibu alieleza kuwa mradi umekwisha Kutambulishwa kwa Wadau katika wilaya zote saba za Mkoa wa Dodoma.
2. Kutoa Mafunzo kwa viongozi wa Serikali za Vijiji kumi na Kimoja vya Wilaya ya Kongwa na Mpwapwa: Idadi ya Viongzo waliopata Mafunzo ni 422 ikiwa Wanawake 109 na wanaume 313.
3. Kutengeneza na Kusambaza vifaa vya Utawala Bora na Demokrasia katika vijiji 11 vya Mradi:
4. Kutengeneza na kusamabaza vifaa vya Elimu Mradi kwa walengwa wa Mradi
5.Kuandaa Matangazo na Vipindi vya redio.
6. Ufuatiliaji na tathmini: Mratibu alifafanua kuwa ufatiliaji uliokwisha kufanywa imeonyesha kuwa uelewa wa viongzo hasa kwenye masuala yanayohusu utawala bora na demokrasia umeongezeka ikilinganishwa na kabala ya Mafunzo
Katika kuhitimisha taarifa yake ya utekelezaji Mratibu huyo wa Mtandao Ndugu Edward Mbogo aliziomba Halmashauri za Serikali za Mitaa kuunga mkono juhudi zilizofanywa katika kukuza demokrasia na utawala bora hasa katika kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Kwa upande wake Mgeni rasmi Bi. Josephine Pamela ambae pia ni Mjumbe wa Bodi ya NGONEDO aliipongeza NGONEDO na Halmashauri zote za Wilaya kwa mapokeo yao ya Mradi huu. Aliwasisitiza Maafisa Maendeleo kutoa ushirikiano mkubwa hasa kwa kuwa Asasi za Kiraia zimebeba jukumu ambalo ki Msingi lilipaswa kutekelezwa na Halmashauri.
Kwa upande wa Washiriki, Ndugu Makundi ambae ni Mratibu wa Mtandao wa Asasi za Kiraia Wilaya ya Chamwino alieleza kufurahishwa na jinsi utekelezaji ulivyo shirikishi hasa kwa kuyafikia makundi yaliyo vijijini. Pia alitoa ushauri kuwa Halmashauri zote zishiriki kikamilifu katika kuifanya Miradi kama hii ili iwe endelevu kwa ustawi wa jamii.
NGONEDO inatekeleza Mradi huu katika wilaya za Kongwa, Bahi, Kondoa, Chamwino, Mpwapwa, Chemba, Kondoa na Doodoma Mjini, Mradi huu unategemewa kuwafikia viongozi takribani 1580 katika vijiji 42 vya mkoa wa Dodoma na wananchi wa kawaida takribani 350,000 kwa kipindi cha miaka miwili.
William Lucas-Afisa Mradi (Mawasiliano)
Ngo Ngonedo's blog
Habari na Picha kwa Wadau
Monday, 29 June 2015
Thursday, 11 June 2015
Ngo Ngonedo's blog: MAONI: Leo ni Bajeti, ni muhimu kuisikiliza, kuielewa
www.ngonedo.org
Watanzania leo wanaelekeza macho na masikio yao mjini Dodoma,
kusikiliza Hotuba ya Bajeti ya Serikali, inayotarajiwa kusomwa saa 10
jioni bungeni na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya.
kusikiliza Hotuba ya Bajeti ya Serikali, inayotarajiwa kusomwa saa 10
jioni bungeni na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya.
Tayari Waziri Saada alishaeleza kuwa bajeti ya
mwaka wa fedha wa 2015/16, inatarajiwa kuwa ya Sh22.480 trilioni, kwa
matumizi ya kawaida na maendeleo. Ni jambo lililo wazi kwamba bajeti ni
mpango au mkataba wa namna Serikali itakavyokusanya na kutumia fedha za
wananchi.

Jambo muhimu katika bajeti ni namna Serikali
inavyotumia fedha katika vipaumbele na mipango mbalimbali. Tunafahamu
kuwa bajeti huandaliwa na kutekelezwa kwa kipindi cha mwaka wa fedha,
badala ya mwaka wa kalenda. Kwa Tanzania, mwaka wa fedha huanzia Julai
hadi Juni 30 wa mwaka unaofuata. Mchakato wa bajeti ni mzunguko
unaoendelea mwaka mzima.

Bajeti inahusu fedha au rasilimali za wananchi,
kwa hiyo inatupatia dirisha la kufahamu umakini wa kweli wa Serikali
katika utatuzi wa matatizo mbalimbali ya wananchi katika juhudi za
kuleta maendeleo.
kwa hiyo inatupatia dirisha la kufahamu umakini wa kweli wa Serikali
katika utatuzi wa matatizo mbalimbali ya wananchi katika juhudi za
kuleta maendeleo.
Hivyo basi ushiriki wa wananchi kuanzia mchakato
hadi katika mjadala bungeni kupitia wawakilishi wao, utaboresha
uwajibikaji, kuzuia fursa za rushwa na kusimamia matumizi endelevu ya
rasilimali za umma na hatimaye kusaidia kuondoa matatizo yanayoikabili
jamii ikiwamo umaskini.

Kwa upande mwingine, wananchi wana umuhimu mkubwa
katika suala la bajeti, kwani mamlaka yote ya Serikali na viongozi wa
umma hutoka kwa wananchi. Hii ina maana kuwa wananchi ndiyo wenye
mamlaka makubwa zaidi ambayo hutoa uhalali na mamlaka kwa Serikali na
vyombo vyake.

Vivyo hivyo, rasilimali zote za Taifa na ugawaji
wake kimatumizi, vinakuwa chini ya wananchi. Wananchi ndiyo wanaolipa
kodi na kutoa michango mbalimbali inayoiwezesha Serikali kutekeleza
mipango ya maendeleo.
wake kimatumizi, vinakuwa chini ya wananchi. Wananchi ndiyo wanaolipa
kodi na kutoa michango mbalimbali inayoiwezesha Serikali kutekeleza
mipango ya maendeleo.
Kwa mantiki hiyo, wananchi ndiyo wenye masilahi na
rasilimali zao, kwa mustakabali wa nchi yao, hivyo shauku ya kushiriki
suala la bajeti na utekelezaji wake, ni suala la msingi kwa kila
mwananchi kulizingatia.
rasilimali zao, kwa mustakabali wa nchi yao, hivyo shauku ya kushiriki
suala la bajeti na utekelezaji wake, ni suala la msingi kwa kila
mwananchi kulizingatia.
Takwimu zinaonyesha kuwa karibu asilimia 80 ya
wananchi wote wa Tanzania ni wakulima, wafugaji wadogo na wa kati. Hivyo
ni muhimu kwa kundi hili kuzingatia mamlaka yake na kushiriki
kikamilifu katika kuisikiliza na kuielewa bajeti itakayowasilishwa
bungeni leo na Waziri Mkuya.

Hatua hiyo itawasaidia kuilewa kwa kusikiliza wenyewe badala ya kuhadithiwa, kuichambua na kuitathmini kwa mapana na marefu.
Huu ni mwaka wenye mambo mengi ya kitaifa, mbali
na shughuli za maendeleo, pia kuna uandikishaji wa Daftari la Kudumu la
Wapigakura, vitambulisho vya Taifa na Uchaguzi Mkuu, mambo yote hayo
yanahitaji kujadiliwa kwa umakini, lakini mjadala wenye afya utatokana
na usikilizaji makini wa hotuba ya bajeti.

Usilikizaji wa bajeti ni njia ya kumuongezea
uwelewa mwananchi wa kawaida, kujua katika eneo lake kuna mipango ipi ya
maendeleo na imetengewa kiasi gani ili waweze kuhoji kwenye mikutano,
mfano, Kamati za Maendeleo ya Kata (WDC), mikutano ya maendeleo ya jimbo
na vilevile, katika halmashauri zao.

Lakini pia ndani ya Bunge, kumekuwa na lawama kwamba mijadala ya
bajeti mara nyingi hujikita katika ushabiki wa kisiasa, kupigana
vijembe na hata Bajeti Mbadala ya Kambi Rasmi ya Upinzani, huzodolewa
kwamba ni ‘bajeti ya harusi’ na kauli nyingine nyingi za kejeli.
bajeti mara nyingi hujikita katika ushabiki wa kisiasa, kupigana
vijembe na hata Bajeti Mbadala ya Kambi Rasmi ya Upinzani, huzodolewa
kwamba ni ‘bajeti ya harusi’ na kauli nyingine nyingi za kejeli.
Bajeti hii ambayo ni ya mwisho kwa utawala wa Rais
Jakaya Kikwete ni vyema ikawa mfano kwa kusikilizwa kwa umakini na
kujadiliwa kwa hoja, pia kwa ni jambo la muhimu kwa wabunge kutulia
bungeni hadi wakati wa kuipitisha, kwa kujenga hoja na kuwasaidia
wananchi kuielewa wakati wa mjadala.

Wednesday, 27 August 2014
Kikwete awaita Ukawa Ikulu
RAIS Jakaya Kikwete amesema yupo tayari kukutana na viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ili kunusuru mchakato wa Katiba mpya.
Bunge lajigeuza Tume ya Warioba
Dodoma.
Kitendo cha Bunge Maalumu la Katiba kukusanya maoni ya makundi na wananchi mbalimbali,kimepokewa kwa hisia tofauti, baadhi ya wasomi wakisema ni kinyume cha sheria na kuonyesha
kutapatapa huku Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba
akisema linafanya kazi ambayo tayari tume yake ilishaifanya.
Tuesday, 26 August 2014
Peter Michael Mabula posted in UWANJA WA DINI - RELIGIOUS FORUM
Peter Michael Mabula | 6:09am Aug 26 |
KANISA LA KRISTO NI WATU GANI?
BWANA YESU asifiwe ndugu.
Karibu tujifunze kuhusu kanisa la KRISTO duniani.
Kanisa la KRISTO ni kundi la watu ambao.
1. Wamekombolewa kwa damu ya YESU KRISTO.
Waefeso 1:7-‘’Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake. ‘’
2. Wametengwa na dunia.
2 Kor 6:16-18-‘’ Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, ‘’
3. Huamini injili.
Yohana 20:31- ‘’ Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. ‘’

Subscribe to:
Posts (Atom)